NJOMBE; Nawaomba waumini tushirikiane kukemea vitendo vya ukatili katika familia

0

 Dawati la jinsia na watoto polisi wilaya ya njombe Latoa elimu Kuhusu malezi ya watoto katika kanisan la katoliki njombe.


Mkuu wa dawati la jinsia wilaya ya Njombe mkaguzi msaidizi Mary kweka akiambatana na mkaguzi kata ya njombe mjini mwema Florida kiecha wametoa elimu Kuhusu kushirikiana na jeshi na kuangalia malezi ya watoto.

Akizungumza amesema malezi ya watoto yamekuwa sio mazuri ndio maana watoto wetu wamekuwa wakijihusisha na vitendo vya jinsia Moja ambavyo ni kinyume na maadili

Vile vile amewahasa wahumini njombe kuendelea kuwalinda watoto ambao ndio taifa kesho.

Kwa upande wake mkaguzi kata ya njombe frolida amesema Wananchi waendele kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kutoa taarifa za wahalifu na uhalifu pia waepuke kujichukulia Sheria mkononi

Nae fr chengula ambae ni paroko wa parokia hiyo amewashukuru jeshi la Polisi mkoa wa kwa kuendelea kutoa elimu ili jamii kwa ujumla itambue vitendo ambvyo ni kinyume maadili yetu

Aidha jumla wahumini zaidi ya elfu Moja wamepata elimu Kuhusu malezi ya watoto kutoka dawati la jinsia na watoto wilaya njombe ambao walisali Misa ya Kwanza na pili.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 
#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top