Radi yaua na kujeruhi wanafunzi 44 mkoani Lindi

0

Mwanafunzi mmoja anayejulikana kwa jina la Alex Justine Manyela mwenye umri wa miaka 18 kidato cha Nne wa shule ya sekondari kipaumbele amefariki April 24, 2023 baada ya kupigwa na radi akiwa darasani na wanafunzi wenzanke wakiendelea na mitihani ya kujipima ngazi ya wilaya.


Akidhibitisha kutokea kwa kifo hicho mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo alisema kuwa ni kweli radi limesababisha kifo cha mwanafunzi mmoja anayejulikana kwa jina la Alex Justine umri 18 na wengine 44 wamejeruhiwa.

Mhe. Moyo alisema kuwa jumla ya wanafunzi wa kike 34 wamejeruhiwa na wanaendeleza vizuri huku majeruhi wa kiume wakiwa 11 huku mmoja wao akifariki kabla ya kufikishwa Hospitali ya wilaya ya Nachingwea.

Kwa upande wake kaimu Mganga Mkuu wilaya Dkt Ramadhan Maige alisema kuwa majira ya saa tisa na nusu alipokea simu kutoka kwa afisa elimu sekondari juu ya kutokea kwa ajali iliyotokana na radi.

Dkt Maige alisema kuwa walipokea majeruhi 45 kutoka katika shule ya sekondari Kipaumbele huku mwanafunzi mmoja akiwa tayari ameshafariki.
chanzo: Nachingwea fm
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 
#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top