Rais Samia Suluhu Hassan amevunja Bodi ya Shirika la Reli la Tanzania (TRC), Aidha, ametengua uteuzi wa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ndege za Serikali (TGFA), Mhandishi John Nzulule.
Kwa mujibu wa taarifa iliyosainiwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Zuhura Yunus Jumapili Aprili 9, 2023 imeeleza kuwa Rais Samia amemtaka Katibu Mkuu Kiongozi kuwaelekeza Makatibu Wakuu wa Watendaji Wakuu kusoma ripoti hiyo, kujibu na kuzifanyia Kazi hoja zote.
