Rais wa Kenya William Ruto ametaka kukamatwa na kufunguliwa mashtaka kwa mhubiri mwenye utata Paul Mackenzie ambaye aliwataka wafuasi wake kufunga hadi kufa.
![]() |
President Dr William Ruto |
Polisi nchini Kenya imesema madhehebu ya itikadi kali ya Kikristo yamesababisha vifo vya takriban watu 60. Wahanga walilazimika kufunga hadi kufa kwa Imani kwamba wangekutana na Yesu Kristo.
Rais wa Kenya William Ruto ameahidi kwamba msako kabambe
utafanywa dhidi ya kile alichokiita kuwa matendo yasiyokubalika ya kidini.
Amesema
hayo mnamo wakati polisi wakipata miili zaidi iliyozikwa kwenye kipande cha
shamba ndani ya msitu wa Shakahola kaunti ya Kilifi, Pwani ya Kenya.
Polisi wamemtaja mhubiri anayeshukiwa kuwapandikisha waumini hao misimamo hiyo mikali kuwa ni Paul Mackenzie Nthenge.