Serikali yaagiza mishahara ya watumishi ianze kulipwa kabla ya Eid El Fitr

0

 Watumishi wa serikali Zanzibar wataanza kupokea mishahara yao ya mwezi wa nne kuanzia leo baada ya Rais na Mwenyikiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Hussein Ali Mwinyi kuagiza mishahara hiyo ilipwe.


Kwa mujibu wa taarifa ya Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais - Ikulu, Charles Hilaly ya Aprili 16, 2023, Rais Mwinyi ameelekeza kufanyika mapema malipo ya mishahara ya wafanyakazi wa Serikali kwa ajili ya matayarisho ya Sikukuu ya Eid El Fitr.

Sherehe hizo zinatarajiwa kuangukia kati ya Ijumaa au Jumamosi ya Aprili 21 au 22, 2023 na Rais Mwinyi anataka wafanyakazi Serikalini kuwa na muda wa kutosha kufanya maandalizi ya sherehe za Eid El Fitr.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 
#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top