Sura ya Biblia iliyofichwa yagunduliwa tena baada ya miaka 1,750

0

 Sura  hiyo iliyofichwa ya maandishi ya Biblia ambayo inasemekana kuwa ya zamani miaka 1,750 imefasiriwa na mwanasayansi wa Austria,  maandishi hayo yanashukiwa kuwa yalitokea katika karne ya 3 kabla ya kunakiliwa katika karne ya 6 kulingana na uchunguzi uliochapishwa mwezi uliopita katika jarida la New Testament Studies.


Grigory Kessel, mtaalamu wa enzi za kati kutoka Chuo cha Sayansi cha Austria, alitumia upigaji picha wa ultraviolet

 ili kuchanganua tafsiri ya Kisiria ya Mathayo sura ya 11 na 12 ya Biblia chini ya aya tatu za maandishi katika hati hiyo.

“Hadi hivi majuzi, ni hati mbili tu zilizojulikana kuwa na tafsiri ya Syria ya Kale ya injili.”

Ilikuwa vigumu kupata ngozi katika Enzi za Kati, kwa hiyo hati-mkono zilipofutwa, karatasi hiyo ilitumiwa tena na watafiti wanasema wasomi walikuwa tayari wanafahamu hati hiyo mwaka wa 1953 na Iligunduliwa tena mwaka wa 2010 kabla ya kuwekwa kidijitali mwaka wa 2020. 

Kupitia mwangaza wa asili na picha za UV Phys.org ilisema kwamba ingawa Kigiriki cha awali cha Mathayo sura ya 12, mstari wa 1 husomeka hivi: “Wakati huo Yesu alipita katikati ya mashamba siku ya Sabato, wanafunzi wake wakawa na njaa, wakaanza kuchuma masuke, wakala,”       

     tafsiri mpya ya Kisiria yasema, “[…] wakaanza kuchuma masuke, wakayasugua mikononi mwao, na kuyala.”

Kati ya nyaraka mbili zinazojulikana kuwa na tafsiri ya Kisiria ya Kale ya injili, moja imehifadhiwa katika Maktaba ya Uingereza huko London na nyingine katika Monasteri ya St. Catherine kwenye Mlima Sinai, nyumba ya watawa kongwe zaidi ulimwenguni inayoendelea kufanya kazi na ya tatu ilitambuliwa hivi majuzi kupitia Mradi wa Sinai Palimpsests kutumia taswira kurejesha maandishi yaliyofutwa kutoka kwa maandishi katika maktaba ya St. Catherine.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 
#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top