Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imelani Mapigano yanayoendelea Nchini Sudan na imezitaka pande zote mbili zinazohasimiana kutatua mgogoro huo kwa majadiliano ya amani na usalama
Hayo yamesemwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano Mhe. Dkt. Stergomena Tax wakati akitoa taarifa Bungeni aprili 19,2023
Mhe. Dkt. Stergomena amesema Tanzania imesikitishwa na hali ya kuzorota kwa amani na usalama inayoendelea Nchini humo
Mhe. Dkt. Stergomena amesema Serikali imeendelea kufanya mawasiliano ya mara kwa mara na Balozi wa Tanzania uliopo Khartoum ili kujua hali inavyoendelea na kuna watanzania takribani 210 ambao 171 ni wanafunzi na wengine ni maafisa wa ubalozi na raia wengine na hadi sasa hakuna mtanzania yoyote aliyeripotiwa kuathirika na mapigano hayo