Katika hali isiyokuwa ya kawaida watu wasiojulikana wamebomoa stoo ya
chakula cha wanafunzi wa shule ya msingi Tandala iliyopo wilayani Makete mkoani
Njombe na kufanikiwa kufanya wizi.VIDEO TAZAMA HAPA CHINI👇👇
Tukio hilo linadaiwa kutokea usiku wa March 22 mwaka huu ambapo watu hao walianza kubomoa ukuta na baada ya kushindwa kutoboa ukuta huo walikwenda kubomoa mlango na kufanikiwa kuingia ndani ya stoo hiyo,hivyo kufanikiwa kutekeleza tukio hilo la wizi.
Akizungumza na Green fm ofisini kwake Aprili 12,2023 Mwalimu mkuu wa shule
hiyo Simon Haule amesema alizipokea taarifa hizo na kueleza kuwa watu hao
walifanikiwa kuiba debe 20 za mahindi na lita lita 20 za mafuta ya kupikia na
hivyo kupelekea upungufu wa chakula katika shule hiyo.
Mwl.Haule amesema tukio hilo sio la kwanza kutokea katika shule hiyo kwani
miaka kadhaa nyuma yametokea matukio mengine ya wizi wa chakula pamoja na wizi
wa vifaa vya shule ikiwemo komputa .
mwenyekiti wa kamati ya chakula katika shule ya Msingi Tandala Kastory
Sanga amesema kuwa tukio hilo ni la aibu kuona watu wanaiba chakula kwa ajili
ya watoto huku akisema kuwa anaamini waliohusika katika tukio hilo ni wazawa
kwani watu waliofanya tukio hilo wangelikuwa sio wenyeji wangeanza kubomoa
ofisi za walimu lakini cha kushangaza walianza kubomoa jengo la stoo ya
chakula.
Mwenyekiti wa kijiji cha Tandala Yusuph Ilomo amesema kuwa sababu ya kuendelea kwa matukio ya wizi katika shule ya msingi Tandala ni kutokuwepo kwa mlinzi.
baadhi ya wazazi wameeleza kusikitishwa na tukio hilo walilodai si la kibinadamu kwani chakula hicho kimekuwa kikichangiwa na wazazi kwa ajili kuwafanya watoto wapate chakula shuleni.