VIKUNDI VYA ULINZI SHIRIKISHI WAMETAKIWA KUZINGATIA UKAMATAJI SALAMA.

0

Vijana wa vikundi vya ulinzi shirikishi wametakiwa kutotumia nguvu kupita kiasi katika kutekeleza majukumu yao ukamataji badala yake kuzingatia ukamataji salama.


Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SACP. Muliro J. Muliro ameyasema hayo tarehe 12. 04. 2023 wakati wa ufungaji wa mafunzo ya Polisi Jamii katika viwanja vya Tanganyika Pakers, Kinondoni, Jijini Dar es Salaam.

SACP Muliro amesema "hatutegemei kuona mtu aliyekamatwa na vikundi vya ulinzi shirikishi kukutwa amevunjika mkono au mguu kwaama nyinyi mmeshafundishwa namna ya ukamataji salama.

Aidha, SACP. Muliro amevitahadharisha vikundi vya ulinzi shirikishi kutoshona au kuvaa sare zinazofanana na Jeshi lolote ambalo lipo kisheria hapa nchini.

Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, ACP Mtatiro Kitinkwi amewapongeza wazazi na walezi kwa kuwaruhusu vijana wao kuhudhuria mafunzo hayo ya ulinzi shirikishi.

Mafunzo hayo yamewezeshwa na Kiongozi wa Kanisa la Inuka Uangaze, Nabii na Mtume Boniface Mwamposa na kuhusisha vijana 225.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 




#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top