Wanafunzi msijaribu kuficha vitendo vya ukatili mnavyofanyiwa

0

 Jeshi la Polisi Wilaya ya Makete limewataka wanafunzi kutoa taarifa kuhusu vitendo vya ukatili vinavyotokea maeneo ya shule na majumbani.


Inspekta Hussein Lujendo akiwa na timu ya Dawati la Jinsia na Wataalamu kutoka Ofisi ya Ustawi wa Jamii Wilaya ya Makete wametoa Elimu kuhusu ukatili wa Kijinsia kwa wanafunzi shule ya Sekondari Iwawa Aprili 18, 2023.

Inspekta Lujendo amesema katika Jamii ya sasa kumekuwa na matukio mengi ya ukatili na kusababisha mmonyoko wa maadili hivyo amewataka wanafunzi kutoa taarifa kwa wazazi, Viongozi wa Mitaa, Ustawi wa Jamii au Polisi ili kudhibiti matukio hayo.

Vilevile amewataka wanafunzi kutoshiriki kwa namna yoyote ile kujihusisha na mapenzi, kutoa mimba kwani kufanya hivyo kutawapelekea kufikishwa mahakamani na kuchukuliwa hatua za kisheria.

Tyson Gavile kutoka Ofisi ya Ustawi wa Jamii Wilaya ya Makete amesema vitendo vya kushiriki mapenzi katika umri mdogo vinapelekea watoto wengi kutofikia malengo na inaweza kuwapelekea kupata magonjwa huku akiwataka kuripoti matukio yoyote ya kikatili yanapotokea

Kaimu Mkuu wa Shule Iwawa Sekondari Mwalimu Jitahidi Sanga amesema Dunia sasa inapitia wakati mgumu unaosababisha madhara makubwa kwa Jamii na kuwataka wanafunzi kuwa makini na mambo ya Dunia.

Zaidi ya Wanafunzi 1,000 wamepata elimu ya ukatili shule ya Sekondari Iwawa ammbao wameshukuru kwa elimu waliyoipata na kuahidi kuwa walinzi na kuhakikisha wanashiriki kikamilifu katika kupambana na ukatili wa kijinsia
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 




#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top