Wanafunzi wawili wafariki dunia wengine 246 walazwa kwa kula chakula shuleni

0

SHULE ya Wasichana ya Sacred Heart Mukumu Girls katika Kaunti ya Kakamega imefungwa baada ya wanafunzi wawili kufariki dunia kwa kile kinashukiwa kuwa ni athari ya kula chakula kibovu na kunywa maji machafu.

Wanafunzi 246 walilazwa katika Hospitali Kuu ya Kaunti ya Kakamega na Hospitali ya Kimehenari ya St Elizabeth wakiwa na matatizo ya kuhara, kutapika na kichefuchefu.

Mkurugenzi wa Elimu eneo la Magharibi Jared Obiero ametangaza hatua ya kufunga shule hiyo leo Jumatatu.

Wanafunzi 25 wangali wamelazwa katika hospitali tofauti.

Seneta wa Kakamega Dkt Boni Khalwale amezuru shule hiyo leo Jumatatu akiwa na Mwakilishi wa Kike wa Kaunti ya Kakamega Elsie Muhanda.

Dkt Khalawe anataka usimamizi wa shule hiyo ubadilishwe.

Maafisa kutoka Wizara ya Afya walikusanya sampuli kutoka shuleni hapo wiki jana na kuzituma kwa maabara ya Taasisi ya Uchunguzi wa Kiafya Nchini (Kemri) lakini matokeo hayajawekwa wazi.

Wazazi walifurika shuleni kuchukua watoto wao baada ya kutokea kwa vifo vya wawili hao.

Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Bi Fridah Ndolo mnamo Jumapili, Aprili 2 aliambia wazazi kwamba walioangamia ni mwanafunzi wa Kidato cha Kwanza W na mwingine wa Kidato cha Pili C.

“Tuwaombeeni wanafunzi na jumuiya ya Mukumu. Tufuatilie matibabu ya watoto vizuri. Tumepoteza wawili…Mungu atupe nguvu kuhimili msiba huu,” akasema Bi Ndolo.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 




#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top