Wananchi Tandala wazikubali gharama mpya za kulipia Maji

0

 Wananchi wa kijiji cha Tandala wilayani Makete mkoani Njombe wamepokea mapendekezo yaliyotolewa ya ongezeko la gharama za kulipia huduma ya maji

Afisa maendeleo wa RUWASA wilaya ya Makete Beauty Sileke akizungumza na wananchi wa kijiji cha Tandala amesema bei zinazopendekezwa na wananchi kulipia huduma za maji hazikidhi uwezo wa kuendesha miradi ya maji kwani inaonesha mwishowe miradi ya maji itakufa kutokana na kukosa fedha za kuiendesha

Amesema kwa wilaya ya Makete wametathmini na kupiga hesabu ya gharama za uendeshaji wa miradi ya maji kwamba kuwe na bei moja ya maji ambayo italipwa na watumiaji ambapo kwa mtu anayetumia maji katika kituo cha jumuia kwa mwezi atalipia shilingi 2000, na mtu aliyeingiza maji nyumbani kwake kwa mwezi atalipia shilingi 3000.

Baadhi ya wananchi Baraka Ilomo, Shaibu Mahenge na Anord Sanga wamekuwa na maoni tofauti kuhusu kulipia huduma ya maji huku wengine wakiona ni afadhali wafungiwe mita ambazo zitasaidia kutibu changamoto zinazojitokeza ikiwemo kudhibiti mivujo ya maji.

Meneja wa RUWASA Wilaya ya Makete Mhandisi Innocent Lyamuya amesema kwa sasa mita za maji zitafungwa kwenye taasisi kama agizo la Waziri wa Maji lilivyosema na kwa mtu binafsi anayehitaji kufungiwa mita kwa hiari yake anatakiwa kuandika barua ya kuomba na wao watamfungia

Gharama hizo mpya za maji zitaanza kutozwa kuanzia mwezi Mei mwaka huu na kuendelea mpaka itakapotangazwa vinginevyo.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 
#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top