Washereheshaji tumieni talanda zenu kukemea ukatili! - Faidha

0

 Washereheshaji nchini wametakiwa kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kukemea na kuwafichua watu wanaofanya vitendo vya Ukatili wa Kijinsia ili kujenga jamii bora.



Hayo yamesemwa na Mratibu wa Dawati la Jinsia na Watoto kutoka Makao Makuu ya Polisi, Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Faidha Suleiman wakati akitoa mada katika mkutano wa chama cha Kisima cha Mafanikio Tanzania unaoundwa na Washereheshaji kutoka mikoa yote Tanzania unaofanyanyika Jijini Dodoma.

ACP Faidha alisema Washereheshaji ni watu muhimu katika mapambano ya ukatili wa Kijinsia kwa kuwa wanakutana na watu wengi hususani katika kazi zao za sherehe mbalimbali.

Alisema tatizo la Ukatili wa Kijinsia linamgusa kila mtu kwa nafasi yake hivyo ni wajibu wa kila mmoja kushirikiana na Jeshi la Polisi kupitia Dawati la Jinsia na Watoto katika maeneo yao ya kazi ili kuhakikisha kuwa vitendo hivyo vinakoma.

Alisema Jeshi la Polisi litaendelea kuchukua hatua mbalimbali za kuzuia vitendo hivyo ikiwemo kutoa elimu kwa makundi mbalimbali ili kuhakikisha linazuia vitendo hivyo na iwapo vikitokea watuhumiwa waweze kukamatwa.
Mkutano huo ukifunguliwa rasmi na Waziri wa Sanaa, Utamaduni na Michezo Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 




#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top