Wasiojulikana wageuza Msitu Dampo...viongozi wa serikali watoa onyo

0

Katika hali ya kushangaza watu ambao bado hawajafahamika wamegeuza msitu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kusini Kati jimbo la Mashariki Kati Tandala kuwa dampo la kutupia takataka.


Kituo hiki kimejionea takataka hizo ikiwemo chupa za bia, maji, za juisi na nyinginezo zikiwa zimetupwa katika msitu huo, ilihali lipo eneo lililotengwa na kijiji cha Tandala kwa ajili ya kutupa takataka.

Katika mkutano wa hadhara wa kijiji hicho uliofanyika wiki iliyopita, wananchi wenye tabia hiyo walionywa na viongozi wa serikali kuacha tabia ya kutupa takataka katika msitu huo na endapo watakamatwa watachukuliwa hatua

Afisa afya kata ya Tandala Odilia Kaishe amekemea vitendo vya watu kutupa takataka ovyo katika msitu huo na kusema vinahatarisha afya za watu hivyo yeyote atakayekamatwa hatua zitachukuliwa dhidi yake

Joseph Shirima ni Afisa Mtendaji wa kijiji hicho amesema tayari hatua zilishachukuliwa za kufukia takataka zilizotupwa hapo ikiwemo pempasi za watoto zilizotumika, na utaratibu unafanyika wa kuziondoa takataka nyingine zilizokuja kutupwa hapo baadaye na kuzipeleka kwenye dampo lililotengwa na kijiji.

Naye Afisa Tarafa ya Lupalilo Augustino Ngailo ameiasa jamii kufuata utaratibu kwa kutupa takataka kwenye vyombo vilivyotengwa ili zikusanywe na kupelekwa kwenye eneo lililotengwa na kijiji huku Mwenyekiti wa Kijiji cha Tandala Yusuph Ilomo akisema wale wanaopewa fedha ili wapeleke takataka dampo wahakikishe wanazifikisha huko na sio kuzitupa njiani ama kwenye maeneo yasiyoruhusiwa.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 




#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top