Wasiojulikana waua mwanamke mwingine kwa kukata viungo vyake!

0

 Milembe Selemani(43), mkazi wa mtaa wa Mseto halmashauri ya mji Geita, aliyekuwa Afisa Ugavi wa Kampuni ya Madini ya dhahabu ya Geita Gold Mine Limited (GGML), amekutwa ameuawa kwa kukatwa viungo vya mwili wake na watu wasiojulikana.


Mwili wa marehemu umekutwa ukiwa umetupwa kwenye moja ya nyumba alizokuwa akijenga zilizopo mtaa wa Mwatulole Kata ya Buhalahala.

Kaimu Kamanda wa Jeshi la polisi mkoa wa Geita Berthaneema Mlay, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo huku watu wanne wakishikiliwa kwa ajili ya uchunguzi.

Akizungumzia kuhusu taarifa hizo, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, ACP Berthaneema Mlay amesema; “Ni kweli tukio hilo limetokea, marehemu ametambulika kwa jina la Milembe Suleiman alikuwa mfanyakazi wa GGM, kitengo cha Ugavi amekutwa ameuawa katika eneo ambalo anajenga nyumba zake.

Eneo ambapo tukio limetokea linaitwa Mwatulole ambazo zilikuwa katika hatua ya ujenzi, mpaka sasa wameshikiliwa watu wanne na uchunguzi unaendelea.

Alipotakiwa kuelezea kuhusu uchunguzi wa awali wa tuko hilo amesema “Yaani hatujabaini chochote mpaka sasa, ndio maana uchunguzi unaendelea,” amesema Kamanda Mlay.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 
#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top