Watu 13 wafariki ajalini Songea-DC Ndile athibitisha

0

 Watu 13 wamefariki dunia na wengine kujeruhiwa kwenye ajali ya gari la mnada aina ya Fuso katika Kijiji cha Namatuhi wilayani Songea mkoani Ruvuma wakitokea Ndongosi Mpakani mwa Tanzania na Msumbiji.

Akithibitisha kutokea tukio hilo Mkuu wa Wilaya, Songea Wilman Ndile amesema ajali hiyo ilitokea jana usiku baada ya gari hilo lililokuwa limebeba wafanyabiashara kuteleza na kutumbukia mtoni.

“Maiti nyingi ni za mjini hapa Lizaboni, Ruvuma na Majengo. Maiti hizo zimehifadhiwa kwenye Hospitali ya Mkoa kwa utambuzi zaidi. Viongozi wanakutana saa nne na watatoa taarifa kamili.” Amesema DC Ndile


Chanzo; Mwananchi.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 
#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top