Watu wanne familia moja wafariki dunia baada ya kuvuta hewa chafu wakiwa usingizini

0

Jeshi la Polisi Kanda Maaalum ya Dar es Salaam limeanzisha Uchunguzi wa tukio la Vifo vya watu wanne wa familia moja ambao wamepoteza maisha baada ya kuvuta hewa chafu ya moshi kutoka kwenye jenereta ambalo waliliwasha ndani ya nyumba na baadae kupitiwa na Usingizi na hatimae kupoteza maisha.


Kwa Mujibu wa Kamanda wa Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam SACP Jumanne Muliro, mkasa huo umetokea  Aprili 19, 2023 maeneo ya Chang'ombe Wilaya ya Temeke.

Akizungumza Jijini Dar es Salaam Kamanda Muliro amesema kulingana na Taarifa za awali ambazo Jeshi la Polisi imezipata ni kwamba Aprili 18 Mwaka huu majira ya saa 4 Usiku usiku watu hao waliwasha Jenereta baada ya umeme kuzimika na kuliweka ndani ya nyumba waliyokuwa Wakiishi.

"Uchunguzi wa awali unaonesha kuwa watu hao walipoteza maisha baada ya kuvuta hewa inayodaiwa kuwa ni hewa chafu ya moshi iliyokuwa inatoka kwenye jenereta baada ya kuwashwa" amesema SACP Muliro.

Kwa Mujibu wa Jeshi la Polisi Waliopoteza maisha ni Kazija Mohamed, Munir Ibrahim, Munira Ibrahim pamoja na Muyyat Ibrahim wakati Mume na mke ambao ni Ibrahim Juma na Aisha Ayubu wote wakiwa ni wakazi wa Kilimahewa,Chang’ombe hali zao sio nzuri na wanaendelea kupatiwa matibabu katika Hospitaliya Taifa ya Muhimbili.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 




#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top