Wawekwa mahabusu kwa kutoshiriki ujenzi wa bweni

0

 Wananchi wawili wanaofahamika kwa majina ya Rehema Chigomwe pamoja na Maria Luoga wakazi wa Kijiji cha Maposeni halmashauri ya wilaya ya Songea mkoani Ruvuma wamelalamikia kitendo cha kuwekwa mahabusu kwa zaidi ya masaa 24 na mtendaji wa kijiji hicho cha Maposeni.


Inaelezwa kuwa wananchi hao waliwekwa mahabusu kwa kosa la kutoshiriki zoezi la kujitolea kuchimba msingi wa bweni la shule ya sekondari ya daraja mbili iliyopo katika Kijiji hicho ambapo serikali imetoa zaidi ya shilingi milioni 140 ya kujengea bweni hilo.

Baada ya kukaa mahabusu zaidi ya masaa 24 mwanamke mmoja ameomba msaada wa kumsaidia mtoto wake maziwa kwakuwa amekatishwa kumnyonyesha mtoto wake baada ya maziwa kuharibika wakati akiwa mahabusu.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 




#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top