Achomwa kisu kisa kelele wakati akihubiri injili

0

 Anord Mpobela ambaye ni Mchungaji wa huduma ya Caanan International Ministry, anayehubiri neno la Mungu katika mitaa jiji la Arusha, amechomwa kisu cha kiganja na mtu anayedaiwa kuwa ni raia wa Misri kwa kilichoelezwa kwamba mtu huyo amekuwa akichoshwa na kelele za mhubiri huyo.


Tukio hilo limetokea siku ya Tarehe Tisa mwezi mei mwaka 2023 majira ya Mchana katika eneo la barabara inayopandisha mtaa wa Jogoo house jijini Arusha,ambapo tayari Mhanga wa Tukio hilo amekwisha wasilisha taarifa hizo kwa jeshi la polisi kwa hatua za kisheria zaidi.

Akizungumza Mchungaji huyo amesema kwamba,"Kwenye habari ya kuchomwa kisu ni lazima niwe na tahadhari kwa sababu sijajua kile kisu kilikuwa na sumu gani, naiomba serikali ituangalie wahubiri wa injili na kwa sababu serikali yetu haina udini, ningefurahi kuona tunapewa ulinzi na vibali vya kuhubiri injili vikatoka kwa wakati sio kuzungushwa,".

Mmoja wa watumishi wa kanisa hilo, amelalamikia uwepo wa changamoto wanayoipata hasa wanapokuwa wakihubiri injili mitaani na kuiomba serikali waitambue kazi yao kwani inao umuhimu katika ustawi wa Taifa
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 
#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top