Ajali ya Bus Njombe mmoja afariki dunia

0

 Basi la abiria kampuni ya Mwalimi lenye namba za usajili T 882 DQE linalofanya safari zake Njombe kwenda Dodoma limepata ajali na kutumbukia kwenye korongo baada ya kugongana na Lori lenye namba za usajili T 260 EAU lililokuwa likijaribu kupita (Overtake) Lori jingine la mafuta katika Mlima wa Ichunilo Mjini Njombe.


Gift Ngalupela ni mmoja wa abiria aliyekuwa amepanda gari hiyo kutoka mjini Makambako wakati ikitoka Dodoma, amesema wakati wakishuka katika mteremko wa Mlima huo Dereva wao aliona Lori mbele wakati likiovertake ambapo aliruka na kuacha basi mpaka lilipogongana na kuacha njia huku likitumbukia kwenye korongo.

Mkuu wa Wilaya ya Njombe Kissa Kasongwa @kissagwakisakasongwa amethibitisha kutokea kwa kifo cha Mtu mmoja aliyekuwa abiria kwenye bodaboda iliyokuwa mbele ya basi, ambaye bado hajatambulika jina lake.

"Tumepokea taarifa ya kifo cha Mtu mmoja na majeruhi kama wawili kwasababu basi halikuwa na Watu wengi,tunaomba Madereva wawe makini sana ukizingatia barabara yetu hii ni nyembamba lakini ajali nyingine zinatokana na uzembe kama tulivyoona hapa magari zaidi ya matatu yanajaribu kupishana."
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 
#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top