Ajali ya ndege yaua Morogoro

0

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za rambirambi kwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Adam Kighoma Malima kutokana na vifo vya watu wawili katika ajali ya ndege.


Ajali hiyo imetokea mei 18,2023 saa 5:30 asubuhi katika kiwanja cha ndege cha Matambwe kwenye Hifadhi ya Taifa ya Nyerere mkoani humo na kusababisha vifo vya watu wawili na majeruhi wawili.

Kwa mujibu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, ndege aina ya Cessina 192 5H-FZS ikiwa na abiria watatu (3) na rubani 1 ilipata ajali wakati ikiruka katika kiwanja hicho.

Katika ajali hiyo askari wawili wamejeruhiwa na hali zao sio nzuri ambapo baada ya kuokolewa walikimbizwa zahanati kwa ajili ya kupata huduma ya kwanza huku wakisubiri ndege ya kuwapeleka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya matibabu zaidi.

Aidha, milli ya marehemu imehifadhiwa kwa muda katika zahanati ya hifadhi hiyo.

Rais Samia amewapa pole wafiwa wote na amesema anaungana na familia hizo katika kipindi hiki kigumu cha majonzi.

Mungu azilaze roho za marehemu wote mahali pema peponi. Amina.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 
#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top