Mkazi wa Iringa, Carlos Mwamilinga mwenye umri wa miaka 37 amekutwa amejinyonga kwa kamba katika chumba alichokuwa akiishi eneo la njia panda ya Mtwivila Mkoani Iringa kwa kile kinachohisiwa kuwa ni kutokana na kutingwa na mawazo kupita kiasi kutokana na kuachana na Mke wake mwezi mmoja uliopita na Mke kuhamia Jijini Dar es salaam.
Wakizungumza baadhi ya Marafiki zake wamesema mara tu baada ya kuachana na Mkewe alikuwa akinywa pombe kali kupita kiasi kutokana na kuwa na mawazo huku Uongozi wa Mtaa ukithibitisha kutokea kwa tukio hilo.
Kwa upande wake Dickson Luhaga ambaye ni Mwanasaikolojia kutoka kitengo cha ushauri nasaha na saikolojia kutoka Chuo Kikuu cha Iringa amesema Carlos alikosa Mtu wa karibu au Marafiki ambao wangeweza kuwa nae karibu pia na kumshauri.
Juhudi za kumpata Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa kupata taarifa zaidi kuhusu tukio hilo bado zinaendelea kufanywa.