Akamatwa kwa kuuza nyama ya Mbwa

0

Mkazi wa Kijiji Cha Igale wilaya ya Mbozi Mkoani Songwe Semeni Shombe (19) amepandishwa kizimbani katika mahakama ya Mwanzo Iyula kujibu shitaka la kuchinja Mbwa na kuuza nyama yake kinyume cha sheria.

Imedaiwa mahakamani hapo na msoma mashitaka Dotto Mwita kuwa April 29 mwaka huu saa 7  mchana alikamatwa  huko katika Kijiji cha Ihowa ambapo alichinja na kuuza nyama ya Mbwa kwa ajili ya matumizi ya chakula kwa wanadamu kitendo ambacho ni kinyume cha kifungu cha 181 cha sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16.

Mshitakiwa huyo amekana shitaka linalomkabiri.

Kwa upande wake hakimu wa mahakama hiyo Mesia Ernest amesema kesi inayomkabili mshitakiwa ni ya

Kugushi chakula kwa lengo la kuuza kinyume na kifungu cha 181 cha sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 huku akijua kufanya hivyo ni kosa.

Hata hivyo kesi hiyo imeahirishwa Hadi Mei 11 mwaka huu itakapotajwa Tena na mshitakiwa ameachiwa kwa dhamana na kuwa na mdhamini mmoja mwenye barua ya utambulisho toka Ofisi ya Mtendaji wake.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 
#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top