Aliyeua kwa makusudi nae kunyongwa hadi kufa

0

Mahakama Kuu ya Zanzibar Mei 15, 2023 imemuhukumu mshtakiwa Khamis Abdulwahab Mahmoud kunyongwa hadi kufa kwa kosa la kumuua kwa makusudi, Mkubwa Juma Khamis mnamo Julai 09, 2008 huko Magomeni Zanzibar.


Akisoma maelezo ya hukumu Jaji wa Mahakama Kuu Zanzibar Mhe. Khamis Ramadhan Abdallah amesema Mahakama imejiridhisha na Ushahidi uliotolewa Mahakamani na kumtia hatiani mtuhumiwa kwa kosa hilo.

Awali Mshtakiwa huyo alishatakiwa kwa kosa la kuua kwa makusudi kinyume na kifungu namba 196 na 197 cha sheria namba 6/2004.

Kesi hiyo ilifunguliwa Mahakamani Disemba 21, 2018 na jumla ya mashahidi nane (8) walitoa Ushahidi wao Mahakamani na kusomwa hukumu hiyo.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 




#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top