ATUHUMIWA KUWADHALILISHA KINGONO WATOTO WATANO.

Hassan Msellem
0

Amour Ali Haji Mwenye umri wa miaka 35 Mkaazi wa kijiji cha Kidemeni Shehia ya Kwale Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba, anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kuwadhalilisha watoto watano wakike na wakiume Kwa nyakati tofauti.

Akisimulia jinsi alivyogundua mjukuu wake kufanyiwa vitendo vya udhalilishaji na kijana huyo bibi wa mtoto mmoja miongoni mwa watoto hao watano, amesema mjukuu wake alikuwa analalamika kuumwa na tumbo mara kwa mara ndipo walipochukua hatua za kumuuliza sababu zinazopelekea kuumwa na tumbo Hilo ndipo aliposema kuwa anakawaida ya kufanyiwa vitendo vya ngono na kijana huyo kwa nyakati tofauti.


"Huyu mtoto Mimi ni mjukuu wangu yani Mtoto wa mwanangu wa kiume naishi nae alikuwa analalamika Sana kuumwa na tumbo Kila siku nilifikia Hadi kumpeleka hospitali lakini hakupata nafuu ndipo nikamuuliza hili tumbo vipi ndipo akaniambia kuwa ka Amour anatuchukua nyumbani kwake Kisha anatulaza na kutuingiza mdudu wake hapo ndipo tukagundua kuwa hawa watoto wanafanyiwa vitendo vibaya na huyo kijana" alisema bibi wa mtoto huyo


Akikiri kupokea taarifa za tukio hilo Sheha wa Shehia ya Kwale Khamis Suleiman Ali, amesema alipigiwa simu na Mkuu wa Wilaya ya Chake Chake Ndugu Abdalla Rashid Ali, kuhusu tukio Hilo na kuombwa kutoa ushirikiano wa kumtia mbaroni mtuhumiwa kazi ambayo ilifanikiwa punde baada ya kupokea taarifa hizo.


Alisema "alinipigia simu bosi wangu (Mkuu wa Wilaya ya Chake Chake) na kunipata taarifa za Hilo tukio na akanitaka tushirikiane kumshika mtuhumiwa ndipo nikashitikiana na askari wa Shehia na kufanikiwa kumtia mbaroni mtuhumiwa" 


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Pemba kamishna msaidizi wa Polisi Abdalla Hussein Mussa, amethibitisha kushikiliwa kwa mtuhumiwa huyo na kusema kuwa upelelezi utakapokamilika mtuhumiwa atafikishwa Mahakamani ili kuendelea na shtaka linalomkabili.


Baadhi ya wazazi ambao watoto wao wanatuhumiwa kudhalilishwa kingono na kijana huyo, wamesema walikuwa wanasikia fununu za Kijana huyo kuwafanyia vitendo vya udhalilishaji wa kingono watoto wa kike na kiume licha ya kwamba hakukuwa na ushihidi wa kutenda makosa hayo Kwa wanajamii kutokuchukua hatua za kumfikisha katika vyombo vya Sheria.


"Tangu zamani tulikuwa tunasikia kuwa huyu Kijana alikuwa na tabia hizi za kuwadhalilisha watoto wa kike na wakiume lakini suala Hilo halikutiliwa maanani kwavile hakukuwa na Mtoto ambaye alimshitakia Mzee wake ilikuwa tunasikia kama fununu tu lakini kutokea kwa hili ndipo tumeamini kuwa ni kweli huyu Kijana ni mkorofi" alisema mmoja wa wazazi ambao Mtoto wake amedhalilishwa kingono na kijana huyo


Tukio Hilo limetokea April 05, 2023 huko katika kijiji cha Kidemeni Shehia ya Kwale Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top