Watu wanne wa familia moja wamefariki dunia wilayani Kilosa mkoani Morogoro baada ya kuungua kwa moto usiku wa kuamkia Mei 5, 2023.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro, ACP Alex Mkama amethibitisha kutokea kwa tukio hilo kusema uchunguzi wa awali umeonesha chanzo cha vifo hivyo ni baba kuichoma moto familia hiyo na yeye akiwemo.
Waliokufa kwenye tukio hilo ni baba wa famlia hiyo, Amani malekela (72) na watoto wake Habibu Amani (10), Sadick Aman na Bahati Amani (5).