BINTI WA MIAKA 13 AJIFUNGUA BAADA YA KUPEWA UJAUZITO NA MZEE WA MIAKA 70.

Hassan Msellem
0

Mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 13 mwanafunzi wa darasa la 5 juzi tarehe 3 May, 2023 aliishangaza familia yake na jamii inayomzunguka baada ya kujifungua, bila ya kuwepo na kiashiria chochote cha uja uzito wake.


Akiwa katika hali ya fadhaa kwa hali iliyomfika mama mzazi wa mtoto huyo amesema kuwa hakuona viashiria vyovyote vya Mtoto wake huyo wa miaka 13 kuwa na ujauzito na badala yake juzi Mei 03 wakati binti huyo anarudi Shuleni alilalamikia kuumwa na tumbo na baada ya muda mfupi akajifungua jambo ambalo lilimfanya mama huyo kupatwa na taharuki na fadhaa.


"Nilikuwa nimekwenda mazikoni Shangafu baada ya kuorudi mazikoni nanikamuona amesharudi Skuli nikamuona analia nikamuuliza una nini akanijibu "aaaa naumi tu mie" nikamwambia basi subiri ni swali ni nikutafutie dawa baada ya kumaliza tu kuswali nasikia kitoto chalia kwanza nikaanguka chini" alisema mama wa binti huyo


Khamis Hussein Abdalla ni mtoto wa mzee ambaye anatuhumiwa kumpa ujauzito binti, amesema ameipokea kwa simanzi kubwa taarifa hiyo kutokana na umri wa mzee wake na binti.


Alisema "Kwakweli sijui hata niseme nini kwasababu yule ni Mzee wangu lakini niseme nimelipokoea kwa simanzi kubwa tukio hili maana kutokana na umri wa mzee na umri wa huyo binti ni sawa na mjukuu wake lakini ndio imeshatokea"


Shaban Rajab Ali, ni mwanajamii wa Shehia ya Kisiwani Sokoni Kwa niaba ya wanajamii wengine, amesema wamesikitishwa sana na tukio kwani walitaraji kuona mzee huyo anasimama kama mzazi kwa binti huyo badala ya kumkatisha ndoto zake za baadae.


"Hili tukio limetusikitisha sana kwakweli kwasababu ukiangalia umri wa huyo mzee na umri huyo binti ni lazima utaacha kunywa wazi ndugu mwandishi, tulitaraji sana kuona yule mzee atakuwa mlezi wa yule binti badala ya kumfanyia vitendo vichafu vya kukatisha ndoto zake alizojiwekea" alisema


Shaaban Salim Mtwana sheha wa Shehia ya Kisiwani, amekiri kutokea kwa tukio hilo na amesema alishirikiana na askari wa Shehia na kufanikiwa kumtia mbaroni mtuhumiwa huyo baada ya binti kuhojiwa na kumtaja mzee Hussein Abdalla Khamis kuwa ndio ambaye alimpa ujauzito huo na kutoa wito kwa wananchi kulaani tukio hilo la kinyama.


Mwandishi wa habari hizi alizungumza na mwalimu wa skuli ya msingi Kisiwani ambayo msichana huyo aliyejifungua anasoma Hamad khamis Hamad, amesema hawakuwahi kuona dalili zote zote zinazoashiria ujauzito kwa msichana huyo huku akidai maendeleo yake ya kimasomo kutokuwa mabaya ukilinganisha na wanafunzi wengine.

 

“Kwakweli hili tukio limetushitua mno kwasababu hatuwahi kuona dalili zozote kwa huyu mwanafunzi na wala hakuonekana kuwa na tabia chafu hapa shuleni n hata maendeleo yake yake ya masomo hayakuwa mabaya sana kwakweli imetuhuzunisha sana” alisema

 

Fat-hiya Mussa Said ni Mratibu wa Chama cha Waandishi wa habari Wanawake Tamwa Kisiwani Pemba, Fat-hiya Mussa Said, ambapo amesema wao kama wanaharakati wa kupinga vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia wamesikitishwa sana na tukio kutokana na umri mdogo wa mtoto ukilinganishwa na umri wa mtuhumiwa. 


“Ni kweli nimepata taarifa za hilo tukio ila kama mwanaharakati ambaye napigania haki za watoto wakike nimeumizwa sana na hilo tukio maana ukiangalia mtoto ni mdogo sana kiasi kwamba hata elimu yake ya msingi hajamaliza na ukiangalia umri wa mzee ni sawa na babu yake sasa kama wazazi ndio wanawafanyia watoto na wajukuu yao matendo haya nani atasalimika” Mratibu Tamwa Pemba


Mtuhumiwa Hussein Abdalla Khamis anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 70 mkaazi wa Shehia ya Kisiwani Sokoni Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba ambae ni fundi wa nyumba za miti kwa sasa anashikiliwa ktk kituo cha Polisi Wete.


Baadhi ya watu wanaomfahamu waliozungumza na mawio wamesema mzee huyo tokea alipomuacha mkewe miaka 30 iliyopita na kubahatika kupata watoto saba hajafunga tena ndoa


Mwisho.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 




#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top