Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, Esther Mahawe amesema anashangazwa na Wanaume wanaojiua kwasababu ya mapenzi wakati Sensa inaonesha kuwa Wanawake wako wengi nchini kuliko Wanaume hivyo wanaweza kuoa zaidi ya Mke mmoja.
DC Mahawe amesema hayo Mei 8, 2023 wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Dkt. Francis Michael ya kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo katika Wilaya ya Mbozi.
DC amesema "Mimi nawashangaa Wababa, ujue kwenye Sensa nyinyi ni wachache kuliko Wanawake sasa unamuuaje Mwanamke au na wewe unaanza kujiua wakati Wanawake wengine wanakusubiri kule ukawaoe?"
"Sisi tunataka hata mchukue mbilimbili au tatutatu lakini wewe unamuua Mwanamke halafu na wewe unajiua kwa sababu ya Mwanamke!, sio sawa Wanaume acheni kuuua Wanawake na kujiua kisa mapenziL
DC pia amewataka Wananchi wa Kata ya Nambozi kuunda vikundi vya ulinzi shirikishi ili kuimarisha ulinzi na usalama kwenye maeneo yao.