DC Kihongosi atakiwa kuwaelewa wananchi wa Urambo hawataki hasira na kupelekeshwa

0

 Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dkt. Batilda Buriani amemtaka Mkuu mpya wa Wilaya ya Urambo Bw. Kenani Kihongosi kwenda kufuatilia hali ya upatikanaji wa chakula Wilayani humo.

Akizungumza mei 25,2023 baada ya kumuapisha Kihongosi, Dkt. Batilda amesema ufuatiliaji huo utasaidia kuwaepusha wananchi na upungufu wa chakula kwa siku zijazo kutokana na tabia yao ya kuvuna na kuuza mazao yote bila ya kuweka akiba ya chakula.

Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Mkoa amemuonya Mkuu huyo mpya wa Wilaya kwamba wakazi wa Urambo hawapendi kupelekeshwa, na kumtaka kuwafahamu na kuwaeleza jambo pasipo hasira na wao watamuelewa.
Kenani Kihongosi aliyekuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi - UVCCM, aliteuliwa juzi na Rais Samia Suluhu Hassan kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Urambo.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 




#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top