Diwani wa kata ya ya Ikuwo wilayani Makete mkoani Njombe amesema kwa sasa wananchi wanalazimika kutumia gharama zao (kujichanga) ili kuifanyia matengenezo barabara ya Ikuwo - Nkenja ili ipitike kwa gari kwa kuwa imeharibika kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.
Akizungumza kwenye kikao cha baraza la madiwani Mei 4,2023 Diwani huyo amesema kwa sasa barabara hiyo haipitiki kwa gari, hivyo kuiomba TARURA kuiangalia kwa ukaribu barabara hiyo ambayo inahitaji matengenezo
Diwani Mwasanga Amesema barabara hiyo ina umuhimu kwa kuwa wananchi huitumia kwa kusafirisha mazao na wao wenyewe wakiwemo wagonjwa wanaofuata huduma za kiafya katika hospitali ya wilaya ya Makete.