Familia hatimaye yakubali kuwazika Mapacha wao

0

 Isaka Rafael (27) Baba wa Watoto mapacha waliozaliwa kabla ya wakati katika Kituo cha Afya Kaliua, Tabora na mmoja wa pacha kunyofolewa jicho moja na ngozi ya paji la uso amesema yupo tayari kuizika miili ya Watoto wake baada ya kuridhishwa na hatua zilizochukuliwa na Serikali.

Isaka amesema licha ya kwamba mwanzoni aligoma kuzika Watoto wake mpaka waliohusika wapatikane lakini maelezo ya RC wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Burian yameleta faraja kwa Familia na wana imani kwamba adhabu stahiki zitachukuliwa dhidi ya Wauguzi waliohusika kunyofoa viungo vya Mtoto wake.

Isaka ameishukuru pia Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu, Wizara ya Afya, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Ofisi ya DC Kaliua, Vyombo vya Habari na Wadau mbalimbali waliosimama nae katika tukio hilo na kuhakikisha haki inapatikana.
Kwa upande wake RC Tabora ameendelea kusisitiza kuwa Wauguzi wanne wa Kituo cha Afya Kaliua watafikishwa Mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili wakati wowote kuanzia sasa kuhusiana na sakata hilo.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 
#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top