Halmashauri ya Wilaya ya Makete na mkakati wa kutoa elimu kwa wafanyabiashara

0

Timu ya Mapato Halmashauri ya Wilaya ya Makete imetoa elimu ya ulipaji ushuru na faini za Mazao mbalimbali ikiwemo Viazi na mbao kwa wafanyabiashara wa Bonde la Mfumbi na Matamba.

Mkuu wa Idara ya Fedha Seben Mwalutamwa akiwa na baadhi ya Wafanyabiashara wa Mazao hayo amewasihi kulipa ushuru kwa hiari pasipo kudanganya ili kujileteaa maendeleo kiuchumi katika Halmashauri ya Wilaya ya Makete.

"Mapato yanayotokana na ushuru mnaolipa kwenye Mazao yanayozalishwa Makete na kusafirishwaa kwenda Mbeya , Dar es salaam, Dodoma na maeneo mengine ndiyo yanayofanikisha utekelezaji wa baadhi ya miradi na shughuli mbalimbali za kimaendeleo katika Kata zetu...lipeni ushuru ili kuepujaa usumbufu".

Kastori Ngonyani ni mmoja ya wataalamu katika timu ya Mapato amesema kumekuwa na baadhi ya wafanyabiashara au madereva wa magari ya mizigo kutaka kukwepa kulipa ushuru au kukwepa faini wanapokuwa wanazidisha kiasi cha mizigo kwenye Magari yao.

Ngonyani amesema kitendo cha kufungasha Lumbesa hakikubaliki na ni unyonyaji kwa Mkulima hususani wa zao la Viazi na pale wanapokutwa wamefanya hivyo watalipishwa faini kulingana na mzigo uliobebwa kuanzia elfu 50 mpaka laki 3
Mbali na kutoa elimu hiyo timu ya Mapato inaendelea kufanya ukaguzi wa vituo au Mageti yake ya ukaguzi yaliyopo ndani ya Wilaya ya Makete kuhakikisha mazao yote yanayosafirishwa yanalipiwa ushuru
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 




#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top