Hospitali inachunguzwa kwa kuwaweka watoto wachanga kwenye maboksi

0

Hospitali ya nchini Afrika Kusini inachunguzwa kwa tuhuma za tukio la watoto wachanga kuwekwa kwenye maboksi badala ya kiangulio ‘incubator’ au vitanda katika jimbo la Kaskazini Magharibi mwa nchi hiyo.

Chapisho katika mtandao wa Facebook ulionyesha sehemu ya watoto wachanga katika hospitali ya jimbo la Mahikeng, wakiwa wamevikwa blanketi za hospitali za rangi ya zambarau na mirija ya kulishia chakula na kuwekwa kwenye maboksi ya kahawia, vyombo vya habari vya ndani vilisema.

Mkuu wa Afya Kaskazini Magharibi Madoda Sambatha, alisema wanachunguza suala hilo ili kubaini ni muda gani watoto hao walikaa kwenye maboksi hayo.

Sambatha aliomba radhi na kutaka utulivu wakati suala hilo likichunguzwa.

Alisema, kutokana na dharura, utaratibu unafanywa ili vitanda vya ziada vipelekwe hospitalini.

Meneja muuguzi wa hospitali hiyo ameripotiwa kusimamishwa kazi.

Waziri wa Afya Joe Phaahla mnamo Jumatatu amelielezea tukio hilo kuwa ni usimamizi duni wa wale wanaosimamia kituo hicho.

Credit:Habarileo

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

JIUNGE NA IDAWA MEDIA SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Telegram na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka IDAWA TV Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube & Jiunge WhatsApp 

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top