IGP Afanya mabadiliko ya Makanda...RPC Njombe naye ahamishwa

0

Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania ,IGP Camillus Wambura Mei 15,2023,amefanya mabadiliko ya Makamanda wa Polisi wa Mikoa kwa kuwahamisha na wengine kupangiwa majukumu mengine.

Katika mabadiliko hayo amemhamisha Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Longinus Alexander Tibishibwamu kwenda Makao Makuu ya Polisi Dodoma.

Nafasi yake inachukuliwa na Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Salum Ramadhani Morcase ambaye alikuwa Makao Makuu ya Polisi Dodoma.

Pia amemhamisha aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Tarime Rorya Kamishna Msaidizi wa Polisi Geofrey Sarakikya kwenda Makao Makuu ya Polisi Dodoma na nafasi yake inachukuliwa na Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Michael Njera ambaye alikuwa Makao Makuu ya Polisi Dodoma.

Aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Hamis Issah amehamishiwa Makao Makuu ya Polisi na nafasi yake imechukuliwa na aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Makuri Imori.


 

 


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 




#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top