IGP Simon Sirro apewa Mkono wa kwa heri polisi

0

Jeshi la Polisi Nchini limemuaga rasmi aliyekuwa Mkuu wa Jeshi hilo Simon Nyankoro Sirro baada ya kumaliza utumishi wake katika Jeshi hilo.

 


Akiongea na waandishi wa habari mei 10 2023 katika Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es salaam DPA Sirro amesema anamshukuru Mheshimiwa Rais na Amiri Jeshi Mkuu Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kumuamini kipindi chote alichokuwa Mkuu wa Jeshi hilo.

IGP Mstafu Balozi Simon Sirro amebainisha kuwa katika utumishi wake atakumbuka mambo Mengi ambayo yalimuumiza kichwa ikiwemo la kuuwawa kwa askari tisa eneo la kibiti Mkoani Pwani.

Sambamba na hilo amewashukuru maafisa na askari wa vyeo mbalimbali katika Jeshi la Polisi Nchini kwa Mchango wao Mkubwa ambapo amesema walishirikiana kuhakikisha wanalinda raia na mali zao katika kipindi alicho ongoza Jeshi hilo.

Pia amevishukuru vyombo vya ulinzi na usalama kwa namna walivyo shirikiana katika kudhibiti uhalifu Nchini.

Vile vile amevishukuru vyombo vya habari na waandishi wa habari kwa namna alivyoshirikiana na vyombo hivyo kuwa hanarisha wananchi maganikio ya kudhibiti uhalifu Nchini.

Mwisho Mheshimiwa Balozi Sirro amewakaribisha watanzania kufika Mchini zimbambwe na kutangaza fulsa mbalimbali zilizopo Nchini Tanzania.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 
#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top