Jamaa afariki akioga Bwawani!

0

 kazi wa Mtaa wa Samina Kata ya Nyankumbu mjini Geita, Daudi Lufungulo (30) amepoteza maisha baada ya kuzama kwenye bwawa la maji wakati akioga.

Akizungumza Mei 26, 2023 mara baada ya mwili wa kijana huyo kuopolewa, Mkuu wa kituo cha Zimamoto na Uokoaji Wilaya ya Geita, Fidelis Wambura amesema uchunguzi wa awali unaonyesha chanzo cha ajali hiyo ni wingi wa tope ndani ya bwawa hilo lenye kina kirefu.

“Hapa inaonekana kuna kina kirefu na vilevile kuna matope, kwa hiyo huyu bwana hatujui alikuwa na lengo lipi alikuwa anataka kuogelea au alikuwa na dhamira nyingine tofauti, nawasihi wananchi wasipende kuoga au kuogelea kwenye madimbwi kama haya tuchukue tahadhari,”amesema Wambura

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Samina, Joseph Kazungu amesema kijana huyo hakuwa mwenyeji wa eneo hilo na kuwa amehamia mtaa huo siku za karibuni na inawezekana hakujua kama dimbwi hilo linakina kirefu.

Shuhuda wa tukio hilo, Golani Simon amesema kijana huyo alifika kwenye eneo la dimbwi na kuwakuta vijana wengine wanafua na kuwaomba sabuni ili aoge na alipopewa sabuni alivua nguo na kujirusha kwenye maji kisha kuzama.

“Mara nyingi hapa huwa tunachota maji tunaoga pembenei lakini yeye alipofika alitukuta tunafua akaomba sabuni na kujirusha majini na hatukuona akiibuka ndio tukaanza kuomba msaada kwa watu waliokuwa karibu ili tuweze kumuokoa lakini hadi anatolewa akawa ameshafariki,”amesema Simon
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

JIUNGE NA IDAWA MEDIA SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Telegram na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka IDAWA TV Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube & Jiunge WhatsApp 

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top