Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya, linamshikilia Musa Pwele(47) mkazi wa Jiji la Mbeya kwa tuhuma za kushiriki tendo la ndoa na mtoto wake wa kumzaa na kisha kumpa ujauzito.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya, Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP, Christina Musyani, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amedai mtuhumiwa amekamatwa Mei 5 mwaka huu.
Amesema Pwele amekamatwa baada ya kumtishia binti yake wa kumzaa kuwa hatampatia huduma ikiwemo mahitaji ya shule na huduma nyinginezo na kutokana na shinikizo hilo alifanikiwa kumbaka mtoto wake.
"Upelelezi wa shauri hili unaendelea na mara baada ya kukamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani ili hatua stahiki zichukuliwe na kuwa fundisho kwa watu wengine," amesema Kamanda Christina.
Aidha Kamanda Christina ametoa wito kwa wadau wa masuala ya kupinga ukatili wa kijinsia kuendelea kutoa elimu ili watu wenye tabia hizo kuacha mara moja kwani vinasababisha athari za kimwili na kisaikolojia kwa mtu mmoja na jamii.