Katibu Tawala Wilaya ya Mkoani Bi Miza Hassan Faki, amezitaka taasisi na jumuiya mbali mbali Kisiwani Pemba kuandaa miradi itakayowawezesha wanawake kuzitambua haki zao ikiwemo kujikomboa uchumi.
Ametoa kauli hiyo katika ufunguzi wa
mafunzo ya siku ya kuwajengea uwezo wanawake na watu wa makundi maalumu katika
masuala ya haki za binadamu huko Skuli ya Sekondari ya Pindua Mkanyageni
Kisiwani Pemba, amesema tafiti zinaonesha bado wanawake wanakabiliwa na
changamoto mbali mbali ikiwemo ukatili wa kijinsia, udhalilishaji pamoja na
muhali.
Kwa upande wake mratibu wa Asasi za
Kiraia Pemba Ashrak Hamad Ali, ameipongeza jumuiya ya wasaidizi wa Sheria
Wilaya ya Mkoani (MDIPAO) kwa kuandaa miradi wa kutoa elimu ya haki za binadamu
kwa wanawake kwani wanawake ndio wahanga wakuu katika vitendo vya uvunjifu wa
haki za binadamu nchini.
Akifunga mafunzo hayo ya siku mbili
afisa Sheria kutoka idara ya Katiba na Msaada wa Sheria Pemba Bakar Omar Ali,
amesema kunzishwa kwa kampeni ya msaada wa Kisheria ya Mama Samia itasaidia kwa
kiasi kikubwa kutoa elimu ya kisheria kwa akina mama.
Afisa Sheria kutoka idara ya Katiba
na Msaada wa Sheria Pemba ndugu Bakar Omar Ali, ameipongeza Jumuiya ya Wasaidizi
wa Sheria Wilaya ya Mkoani (MDIPAO) kwa kuandaa mradi utakaowawezesha wanawake kuzitambua
haki zao ikiwemo kushiriki katika shughuli mbali mbali za kijamii.
Ametoa kauli hiyo wakati akifunga
mafunzo ya siku mbili ya kuwajengea uwezo wanawake na watu wa makundi maalumu
katika masuala ya haki za binadamu huko Skuli ya Sekondari ya Pindua Mkanyageni
Kisiwani Pemba, amesema tafiti zinaonesha kuwa wanawake na watu wenye ulemavu
ndio wahanga wakuu wa vitendo vya uvunjifu wa haki za binadamu nchini ikiwemo
kufanyiwa vitendo vya ukatili na udhalilishaji.
Aidha amesema kunzishwa kwa kampeni
ya msaada wa Kisheria ya Mama Samia itasaidia kwa kiasi kikubwa kutoa elimu ya
kisheria kwa akina mama.
Akiwasilisha mada juu ya watu wenye
mahitaji maalumu, Wakili wa Watoto Bi Siti Habib Mohammed, amesema miongoni mwa
changamoto zinazowakabili watu wenye mahitaji maalumu ikiwemo watu wenye
ulemavu ni pamona na kufanyiwa vitendo vya udhalilishaji sambamba na kuitwa
majina yasiyofaa.
Malik Mohammed Juma mkaazi wa Mkoani, ameiomba jumuiya hiyo kuendelea kupaza sauti za watu wa makundi maalumu ikiwemo watu wenye ulemavu na wasiojiweza ili waweze kupatiwa haki zao za msingi ikiwemo elimu, huduma za afya na lishe.
Naibu Mkurugenzi jumuiya za vijana umoja wa mataifa Mohammed Hassan Ali, amewataka washiriki hao kutokuwa na muhali na woga pindi wanapofanyiwa vitendo vya uvunjifu wa haki za binadamu ili wahusika wa vitendo hivyo waweze kuchukuliwa hatua za kisheria.
Mkurugenzi wa MDIPAO Nassor Hakim Haji, Amewashukuru wafadhili wa mradi huo kwa msaada wake wa kuiunga mkono jumuiya hiyo Kwa lengo la kuwasaidia wanawake pamoja na watu wa makundi maalumu ili kuzitambua haki zao nchini.
Jumla ya wanawake na watu wa makundi maalum 110 kutoka Wilaya ya Mkoani wamepatiwa elimu ya haki za binadamu na haki nyengine kutoka Jumuiya ya wasaidizi wa Sheria Wilaya ya Mkoani (MDIPAO).