Kauli ya serikali kuhusu Umeme wa Makete kutokea Njombe

0

 Naibu Waziri wa Nishati Steven Byabato akizungumza bungeni jijini Dodoma amesema wataangalia suala la ujenzi wa kituo cha kupooza umeme katika wilaya ya Wanging'ombe mkoani Njombe ili umeme unaokwenda wilayani Makete utokee hapo

Naibu Waziri Byabato ameyasema hayo wakati wa kipindi cha maswali na majibu bungeni Dodoma leo Mei 23, 2023 wakati akijibu swali la Mbunge wa jimbo la Makete Festo Sanga aliyetakakujua ni lini serikali itatatua changamoto ya umeme kukatika katika jimbo lake kutokana na umeme wake kutokea mkoani Mbeya badala ya Njombe hali inayosababisha umeme kukatika mara kwa mara 


"Kupitia bunge hili tuliahidiwa kwamba umeme wa Makete Mtabadilisha 'line' kutoka Mbeya kuja Makete ni laini ambayo imechoka na inasumbua kwa muda mrefu na kusababisha umeme kukatika mara kwa mara, mlituahidi kwamba mtajenga 'sub station' wanging'ombe ili wananchi wa makete wachukulie umeme kutokea Njombe, je imefikia hatua gani?" - amesema Mbunge Sanga


Naibu waziri Byabato amesema moja ya changamoto wanayokabiliana nayo kwa sasa ni umeme kusafirishwa umbali mrefu kutoka kwenye chanzo ambapo wamefanya tathmini kupitia Tanesco na wakabaini makundi matatu ambayo ni wale wenye shida zaidi, wenye shida ya kati na kuna wale ambao maisha yanaweza kuendelea.

"Kwa maeneo ambayo yana shida zaidi tunaishukuru serikali ya awamu ya 6 imetupatia pesa bilioni 500 kwa ajili ya kutekeleza mradi unaitwa gridi imara na utajenga vituo vya kupoza umeme 14 katika awamu hii ya kwanza, sasa nimuhakikishie Mh Festo kwamba eneo lake nitakwenda kuliangalia limewekwa kwenye 'category' ipi katika yael maeneo matatu yenye matatizo makubwa, matatizo ya kati, na matatizo ya juu na nitakufahamisha endepo litajengwa kituo cha kupoza umemem kipindi hiki au itajengwa katika awamu inayofuata lakini kabla ya miaka 6 ijayo kuisha tunatarajia kuwa na kituo cha kupoza umeme kwa kila wilaya ili kuondoa tatizo la umeme kusafirishwa umbali mrefu" amesema Naibu Waziri.

credit: Eddy Blog

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 
#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top