Kijana adaiwa kuwafungia wanawake watatu ndani kisha kuwaingilia

0

Juma Msemwa (27) anashikiliwa na Polisi Njombe kwa tuhuma za kuwafungia ndani kwake kisha kuwabaka na kuwalawiti huku akiwa amewafunga kamba na kuwajaza vitambaa mdomoni Wanawake watatu katika Mtaa wa Kihesa Halmashauri ya Mji wa Njombe.

Prisca Mgaya ni Shuhuda aliyefika wakati wa kukamatwa kwa Kijana huyo na akiongea mbele ya DC wa Njombe, Kissa Kasongwa amesema alipata taarifa kwa Dada aliyetoroka kwenye nyumba waliyofungiwa kisha akaenda kuomba msaada dukani kwake akiwa na hali mbaya kwakuwa Juma alikuwa anafanya nao mapenzi siku nzima na alipochoka alizamisha gunzi au tango kwenye nyeti za Wanawake hao.

"Alipofika na kuniambia kuwa ametoroka kwenye nyumba waliyofungiwa na Juma ambaye alikuwa anawabaka, tukaondoka na wenzangu mpaka kwenye ile nyumba tukataka kuanza kuvunja mlango akatoka Kijana.

"Tulipomuuliza yule Binti kama Kijana mwenyewe ni huyu akasema ndio lakini Kijana akaanza kukataa tukampiga kamba na kwenda kwenye vyumba vingine tukakuta vimefungwa tulipovunja chooni tukakuta Wamama wawili wakiwa uchi na huyu tuliyekuwa nae nje ni wa tatu"

DC Kissa Kasongwa amesema tayari Kijana huyo ameshikiliwa na Polisi huku akisikitishwa na kilichofanywa kwakuwa Mwanamke mmoja alikuwa amefungiwa kwa takribani wiki moja akiendelea kufanyiwa vitendo hivyo kila siku; “Mmoja anasema kabakwa kwa saa 11 bila kupumzika.”
"Niwashukuru Wananchi kwa kuwaokoa bila ya huyu mmoja kujinasua huenda leo tungeongea mengine nitoe rai kwa Wanawake kupunguza ujasiri wa kwenda kwa Mwanaume bila kumjua ni nani.”

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 
#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top