Baba amnyonga mwanae mpaka kufa kisa analia mno

0

 Mambo ya kustaajabisha yanazuka kila iitwapo leo, hivi ndivyo unaweza kusema kwani kila kukicha visa vingi vipya na vya kushangaza vinazidi kutokea duniani.


Hii ni baada ya mwanaume mmoja kutoka Zambia kuamua kumnyonga mwanaye akidai analia mfululizo bila kunyamaza.

Kwa mujibu wa Tovuti ya Zambian Observer ya nchini humo, imeripoti tukio hilo kuwa limetokea eneo la Riverview katika Wilaya ya Mazavuka, Mkoa wa Kusini mwa Zambia.

Inadaiwa mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 27, alifikia uamuzi huo wa kumkaba shingo mtoto wake mwenye miezi nane pekee.

Naibu Msemaji wa Polisi wan chi hiyo, Danny Mwale amethibitisha kwamba mama wa mtoto huyo anayeitwa Esther Lwiindi aliamua kumuacha mtoto na baba yake na kwenda sokoni. Aliporudi alikuta mtoto amenyongwa na kufariki dunia.

Alipohojiwa na Polisi mtuhumiwa alisema alimuua mtoto kwa sababu alikuwa akilia mno wakati mama yake alipoenda sokoni.

Kwa sasa mwili huo uko katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Mazabuka huku mshukiwa akiwa chini ya ulinzi wa Polisi akisubiri kufikishwa mahakamani.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 
#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top