Mama ‘amtelekeza’ mtoto, ajilea mwenyewe

0

Kijana ambaye tutamtaja kwa jina moja la baba (kwa sababu za kimaadili") Hamis amesimulia namna anavyojilea mwenyewe baada ya mama yake ‘kutoroka’ na ‘kumtelekeza’ kwa bibi yake mzaa baba na kwenda kusikojulikana.Akitoa simulizi hiyo katika kongamano la siku ya kimataifa ya familia ambalo limefanyika mkoani Mtwara, Hamisi alisema kuwa mama yake aliondoka na kumucha na baba na bibi ambao wote walifariki na kumuacha akijilea mwenyewe.

“Mama angu alitoweka kwenda kusikojulikana na kuniacha na baba ambaye baadae alifariki na kuniacha nikiwa nalelewa na bibi mzaa baba ambaye nae alifariki na kuniacha nikiwa na lelewa na walezi pamoja na jamii”

“Bibi yangu alifanya juhudi kubwa iliniweze kusoma hakujali maisha yake kuwa ni duni kufariki kwake bibi ndio niliona madhara ya kukosekana kwa mshikamano wa kifamilia kati ya baba na ndugu wengine kifamilia katika malezi yangu”

“Leo nayafahamu madhara ya kuishi bila wazazi na kukosekana kwa mshikamano wa familia yanayochochea uvunjifu wa maadili katika jamii zetu. Kiukweli, nilishikwa mkono na shirika lilisilo la kiserikali la FAWOPA na , siwezi jua kama leo nisingekuwa miongoni mwa watoto wanaofanya ajira zisizo na stara,” amesema.

“Watoto ambao tuko katika mazingira hatarishi tunatakiwa kusimama imara na kupigania ndoto zetu ili kujiletea ukombozi wetu sisi tusikatishwe tamaa na halu zetu bali tupambane katika safari ya kuweza kufikia malengo yetu”


Pia aliongeza kusema: “Mwenyezi Mungu akijaalia nitakuwa miongoni watoto watakaojiunga kidato cha tano mwaka huu. Hata hivyo, sijui nitaendaje katika hatua hiyo ya masomo, kwa kuwa naelewa mahitaji ni makubwa, na safari bado ndefu japo nina amini nina nguvu za kuvuka kila kizingiti ili nifikie ndoto zangu.”

 Mkurugenzi wa Shirika lisilo la kiserikali la Faidika Wote Pamoja (FAWOPA) Baltazar Komba amesema kuwa wapo watoto wengi wanaofanana na Hamisi wanahitaji msaada.

“Katika matokeo yake ya kidato cha nne, alipata division two; huwa tunasaidia watoto ambao wapo katika mazingira hatarishi yaani mazingira magumu. Kimsingi wapo wengi na hatuna mfadhili yoyote, kama kuna mdau anaweza kusaidia watoto tunaomba atusaidie,” ameseama Mkurugenzi huyo.

kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanal Ahmed Abbas alisema kuwa kwa mujibu wa taarifa za dawati la ustawi wa jamii, zaidi ya matukio 693 ya ukatili yakihusisha watoto yameripotiwa; huku ya kingono yakiwa 165 wakati ya kutelekezwa matukio 147. Hata hivyo, zaidi ya matukio 20 yamesha tolewa hukumu.

Chanzo;Mwananchi.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 
#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top