Mama na mwanae wauawa shambani,kichanga cha wiki taatu chakutwa kando ya mto kikiwa hai

0

Mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Elina Kivega (33) mkazi wa Mtaa wa Mgodi Mjini Mafinga amekutwa ameuawa yeye na mtoto wake Daud Kigulu (4) shambani alikokuwa ameenda kuangalia mahindi yake huku kichanga Chake Chenye umri wa wiki tatu kikitutwa kando ya mto kikiwa hai.


Akizingumzia tukio hilo Mwenyekiti wa Mtaa wa Mgodi Nausi Kalinga amesema alipokea taarifa za kuwepo kwa tukio hilo la mauaji ndipo alipoongozana yeye na Afisa Mtendaji kwenda eneo la tukio na kukuta mama huyo na mwanaye wamefariki huku mtoto mchanga wa wiki 3 akiwa bado yupo hai.

Shemeji wa marejemu aliyejitambulisha Kwa majina ya Damas Kigulu amesema baada ya kupokea taarifa kwa mdogo wake kuwa mkewe hajarudi nyumbani waliamua kwenda shambani huko usiku wa mane ndipo walipokutana na tukio hilo la kikatili ambapo mtoto mchanga alikutwa ametupwa kando ya mto akiwa bado hai.

Akithibitisha kupokea miili ya marejemu hao Kaimu Mganga Mkuu Hospitali ya Mji wa Mafinga Dokta Amatha Haule amepokea miili hiyo na tayari imehifadhiwa katika chumba maalumu huku akieleza hali ya mtoto kuwa ni salama na mtoto huyo hana changamoto yoyote.

Jeshi la polisi walifika eneo la tukio na kuondoka na miili hiyo ambapo wanaendelea na taratibu za uchunguzi wa kubaini wahisika waliotekeleza tukio hilo.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 




#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top