Na:Henrick Idawa
Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza Limesema linawashikilia watu watatu akiwemo Mganga wa kienyeji kwa tuhuma za kumkata sehemu za siri mwanamke na kuzibanika ili kupata dawa ya uganga.
Akitoa taarifa hiyo kwa wandishi wa
habari kamanda wa Polisi Mkoani Mwanza Wilbroad Mutafungwa amesema walipokea
taarifa za kifo cha mwanamke Esta Lukoni
jina maarufu kifebe (51) mkaazi wa kijiji cha Bugunangala aliyeuwa kwa kukabwa
shingoni kisha kukatwa sehemu zake za siri na mwili wake kutelekezwa katika
shamba la mihogo.
Amesema katika tukio hilo imeonesha
marehemu aliingiliwa kimwili kabla ya mauji hayo ya kikatili.
“Kwani katika eneo la tukio ulipatikana mpira wa kiume uliotumika (condom),tukio hilo lilifanywa na watu ambao hawakufahamika” amesema mutafungwa
Kamanda Mutafungwa amesema jeshi la
polisi baada ya kupata taarifa hiyo waliendelea na kufanya uchunguzi na kufanikiwa
kuwakamata watuhumiwa.
“Watuhumiwa hao tuliwahoji wamekiri
kuhusika na tukio hilo la ukatili baada ya kumbaka marehemu Esta Lukoni,kisha
kumuua na kumkata sehemu yake ya siri”
Amesema katika watuhumiwa hao waliokamatwa yupo mganga wa kienyeji ambaye inadaiwa alipokea sehemu hizo za siri kisha kuzikausha kwa moto na kuzisaga kwa ajili ya matumizi ya uganga kwa imani potofu za kishirikina.
Amewataja watuhumiwa hao kuwa ni “Masunga
mabula (32),Ezekiel Charles (45) na Salome Rafael (32) na watuhumiwa hawa
watafikishwa mahakamani mara uchunguzi utakapokuwa umekamilika”