Mbwa wazua hofu wageuza bata kitoweo wanajificha mapangoni

0

Wakazi wa kisiwa cha Bezi kilichopo wilayani Ilemela mkoani Mwanza wamekumbwa na hofu kutokana na kusambaa kwa mbwa ambao wamekuwa tishio kwao na kwa mifugo wanayofuga kama mbuzi na bata 

Akizungumza kwa niaba ya wakazi hao Anna Masanga amesema mbwa hao wanakula mbuzi na bata na hujificha kwenye mapango yaliyopo katika kisiwa hicho hivyo kuiomba serikali kuangalia namna ya kuwaondoa ili wasizidi kuleta madhara

"Kipindi cha mvua ikiwa inanyesha hawa mbwa wanatoka kule mapangoni wanajua kabisa hawa watu watakuwa wamejikinga kwenye majumba wanakuja kushambulia wale mbuzi na wakati mwingine wanaingia usiku kwenye Mazizi wanashamulia wanakula mifugo na hivi juzi wamekula mbuzi saba hawa mbwa siyo kwamba wanaishi kwenye miji wanaishi kwenye mapango wito wetu tunaomba bwana mifugo waje ili wawauwe hawa mbwa kuna mwaka Fulani walikuja wakawauwa lakini hawakufa"

"Sasa tumekuja hapa kuangalia kuona situation jinsi ilivyo na ili kuweza kuchukua hatua zinazopaswa na kuwatambua wale wamiliki wa hao mbwa na wale ambao hawatakuwa na wamiliki rasmi tuweze kuwachukulia hatua kwa kuwadhibiti na tutawajulisha mamlaka zingine ambazo zinahusika kuweza kuwadhibiti mbwa hawa"

Mkuu wa wilaya ya Ilemela Hassan Masala amefika katika kisiwa hicho na kusema hatua za kuwadhibiti mbwa hao zinaanza mara moja ili kuhakikisha wakazi hao wanaishi kwa amani.

"Nimepokea simu kutoka kwa wananchi juu ya hii changamoto kwetu sisi kiusalama siyo jambo dogo moja mbwa wenyewe ni mbwa pori wakati mwingine wanaweza kuwa na magonjwa kuna kichaa cha mbwa kuna vitu vingi ambavyo ukivipuuzia vinaweza kuleta shida kwahiyo sisi tumelipa hili nafasi kubwa nikasema nije nione namna ya kutafurta suluhu ya jmabo hili"

Credit-Eatv.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 




#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top