MC Misesemo ajiua CCTV Camera zanasa tukio zima!

0

 Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, limesema kwamba Joel Misesemo mkazi wa Mwananyamala Dar, aliyejirusha ghorofani kwenye jengo la Derm Plaza Makumbusho na kufariki dunia hii leo Mei 23, 2023, amejirusha kwa makusudi kupitia dirisha lililopo ghorofa ya saba ya jengo hilo.

Taarifa hiyo imetolewa na Kamanda wa Kanda hiyo SACP Lazaro Mambosasa, amesema mifumo ya kamera ya jengo hilo imeonesha marehemu alivyojirusha, na kwamba gari lake limehifadhiwa na uchunguzi wa kina wa tukio hilo unaendelea.

"Uchunguzi wa awali unaonesha kuwa marehemu alionekana katika jengo hilo tarehe 23, Mei 2023 majira ya saa 11:40 alifajiri na alimwambia mlinzi wa zamu kuwa anaenda kufanya ibada kwenye msikiti uliopo ghorofa ya 15 ndani ya jengo hilo, hata hivyo muda mfupi baadaye alijirusha kutoka juu ghorofani na kuanguka chini," imeeleza taarifa ya SACP Muliro.

Tarifa hiyo imeendelea kueleza, "Aidha mifumo ya kamera ya jengo hilo inamuonesha mtu huyo akijirusha kwa makusudi kutoka ghorofa ya saba kupitia dirishani, mwili wake umepelekwa Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala kwa uchunguzi zaidi," 
Aidha Jeshi la Polisi limepata gari la marehemu aina ya Suzuki lenye rangi ya silver lenye namba za usajili T142 DRM lililokuwa limeegeshwa kwenye maegesho ya magari katika eneo hilo na limehifadhiwa kituo cha Polisi Oysterbay, na kwamba uchunguzi wa kina unaendelea juu ya tukio hilo.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo wameeleza kuwa, baada ya kufika katika jengo jilo majira ya alfajiri alimwambia mlinzi kuwa anakwenda kufanya ibada ghorofa ya mwisho (ghorofa ya 15) ambapo kuna msikoti.

Joel alipamda mpaka ghorofa ya 13 huku akizungumza na simu, baadae alishuka kwenye lift kisha kupanda tena na kuteremka mpaka ghorofa ya 7 akiendelea kuongea ma simu. Baada ya kushuka ghorofa ya saba alijirusha kupitia dirishani na kuanguka chini ambapo alipoteza maisha papo hapo huku chanzo kikiwa hakijafahamika.

Imebainika kwamba Joel Misesemo anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 32-35 pia alikuwa akijishughulisha na shughuli za ushereheshaji (MC).
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 
#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top