Na Mwandishi watu,Dodoma.
Taasisi ya Misa Tanzania imeshauriwa imekupongeza kasi ya utoaji mafunzo ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari katika masuala mbalimbali ili kuepukana uvunjaji wa sheria za nchi na miiko ya tasnia ya habari.
Ushauri huo umetolewa na mkurugenzi wa habari maelezo na msemaji wa serikali Gerson Msigwa kwa niaba ya Naibu waziri wa Habari, Mawasiliano na Tekonolojia ya Habari,mhandisi Kundo Mathew,katika wa uzinduzi wa maadhimisho ya miaka 30 ya taasisi ya vyombo vya habari kusini mwa Jangwa la Sahara Tawi la Tanzania (MISA Tanzania).
Amesema wakati serikali ikiendelea kuboresha mazingira ya vyombo vya habari taasisi za kihabari nazo zinapaswa kujikita katika kutoa mafunzo kwa wanatasnia ili kuwa wabobezi katika uandishi wa masuala mbalimbali.
Mkurugenzi huyo wa habari maelezo pia amewataka waandishi kutumia karamu na sauti zao kuandika mambo mazuri taifa badala ya kuandika mambo mabaya tu Kama vyombo vya mataifa ya magharibu ikiwemo Marekani wanavyofanya huku pia akisema tangu Rais Samia Suluhu Hassan aingie madarakani ameachia Uhuru kwa vyombo vya habari na kufungulia vilivyofungiwa.
"Katika kipindi hiki tunahitaji sana mafunzo kwa waandishi wa habari.Katika program zetu tuimarishe sana mafunzo kwa waandishi wa habari, Misa Tanzania na wadau wengine tutie mkazo sana kwenye mafunzo kwa waandishi wa habari.Mimi ni miongoni mwa wanufaika wa mafunzo kwa wanahabari ambayo yamekuwa yakitolewa na taasisi ya habari ya MISA-Tanzania"amesema Msigwa.
Mwenyekiti wa MISA Tanzania Salome Kitomari amepongeza serikali kwa kuchukua hatua kadhaa zinazowezesha waandishi wa habari kutekeleza majukumu yao kwa kuondoa vikwazo vingi.
Amesema MISA Tanzania imepita kwenye safari ya miaka 30 yenye milima na mabonde na Kisha kuomba kuendelea kuondoa vizingiti vinavyoendelea kukwamisha wanahabari kufanya majukumu yao.
"Tuna mengi ya kujivunia ikiwemo kuwa na Ofisi yetu eneo la Kinondoni Mkwajuni, Dar es Salaam na kubaki kwenye DNA ya MISA ya Uhuru wa kujieleza, uhuru wa vyombo vya habari na upatikanaji wa taarifa nchini.Wanachama kutoka taasisi na mwanachama mmoja mmoja,Viongozi waliopita wenye mchango kubwa kwenye tasnia ya habari na Wadau wa Maendeleo kutoka serikali za Canada, Finland, Uingereza, Ujerumani, Marekani na nyinginezo"amesema Kitomari.
Kuhusu suala la mafanikio Kitomali ameeleza kuwa tangu kuanzishwa kwa MISA-TAN miaka 30 iliyopita imeweza kutoa mafunzo kwa maelefu ,kuanzisha vituo vya radio na mengine mengi ikiwemo uandishi wa habari za COVID-19.
Naye Mkurugenzi wa MISA Tanzania, Elizabeth Riziki amesema Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Jangwa la Sahara,Tawi la Tanzania (MISA Tanzania), inaadhimisha miaka 30 tangu kuanzishwa kwake, MISA ilizaliwa mwaka 1993 baada ya kikao cha wanahabari waliokutana Windhoek, Namibia kujadili mambo mbalimbali yaliyokuwa yanaukabili Ukanda wa Nchi za Kusini.