Jeshi la Polisi mkoani Arusha linawashikilia watu 12 kwa tuhuma za kufanya vurugu pamoja na uharibifu wa vitu mbalimbali na kusababisha mtu mmoja kufariki dunia maeneo ya Mto wa Mbu Wilayani Monduli.
Katika Taarifa iliyotolewa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha ACP Justine Masejo na kufafanuliwa na Kamishna wa Uhifadhi TANAPA William Mwakilema amesema tukio hilo limetokea Mei 22, 2023 muda wa saa 5:40 asubuhi huko katika Kitongoji cha Magomeni kijiji cha Jangwani eneo la Mto wa Mbu Wilaya ya Monduli Mkoa wa Arusha.
Kamishna Mwakilema amesema Askari wa hifadhi ya Manyara wakiwa katika doria ya kawaida eneo la ziwa Manyara walikamata Wavuvi watatu waliokuwa wakivua samaki katika maeneo yaliyozuiliwa kwa uhifadhi.
Kamishna wa Hifadhi za Taifa TANAPA William Mwakilema amefafanua kuwa umati wa watu hao walikwenda hadi kwenye ofisi ya kijiji cha Jangwani na kufanya uharibifu mkubwa katika ofisi hiyo ya serikali kwa kuvunja madirisha pamoja na kuchana bendera ya Taifa na kuondoka nayo kwa madai kuwa wavuvi wenzao wamezamishwa maji wakati wanakamatwa na Askari wa uhifadhi.
Aidha baada ya uharibifu huo, kundi hilo liliamua kuelekea ofisi na makazi ya Askari wa TANAPA yaliyopo Mto wa Mbu, lakini wakati wakiwa njiani walivamia ofisi na makazi ya Askari wa TANAPA na kufanya uharibifu mkubwa wa magari kwa kutumia marungu na mawe pamoja na kupanga mawe barabarani kuzuia watumiaji wengine wa barabara