Mtoto amuua mama yake kwa kumnyima Chai

0

Mwanamume mmoja amemuua mamake kwa kumchinja baada ya kunyimwa kikombe cha chai katika kijiji cha Alupe, wilayani Busia, katika nchi jirani ya Uganda.


Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini humo, Robin Barasa alimchinja mamake mwenye umri wa miaka 53 kutumia panga baada ya kunyimwa chai mnamo Jumatano asubuhi.

Umati wa watu wenye hamaki ulishambulia Robin na kumpiga kwa mawe hadi kuaga dunia kwa kosa la kumkata shingo na kumuua Pelvine Barasa.

Kwa mujibu wa ripoti ya kituo cha redio cha Emuria FM, mama huyo aliamua kumnyima chai mwanawe baada ya kukataa kulima shamba la mahindi.

Babake Robin na mumwe Pelibe - Robert Ongaria alisimulia kuwa aliondoka nyumbani kwenda kazini katika Hifadhi ya Maiti ya Alupe lakini akapigiwa simu na mwenyekiti wa kijiji kuwa nyumbani kwake kulikuwa kumeharibika.

Ghasia na mayowe yalivutia wanakijiji ambao walitembea mpaka nyumbani kwa Pelvine na kumkuta ameuawa katika shamba la mahindi.

Kulingana na wanakijiji, Robin alimfuata mama yake nyuma ya nyumba, akamdhibiti na kumkata shingo kwa kutumia panga kabla ya kuitupa.

Viongozi katika Jumuiya ya Alupe wamekemea tukio hilo na kuwataka vijana kuepuka matumizi ya dawa za kulevya.

Maiti za wanafamilia hao wawili zimepelekwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti wakati uchunguzi unafanywa na mamlaka za Uganda.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

JIUNGE NA IDAWA MEDIA SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Telegram na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka IDAWA TV Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube & Jiunge WhatsApp 

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top