Mtoto mwenye mchanganyo wa DNA za watu 3 azaliwa Duniani

0

 Mtoto wa kwanza aliyezaliwa na DNA kutoka kwa Wazazi watatu amezaliwa Nchini Uingereza na utaratibu huu ulifanyika ili kuzuia magonjwa ya kurithi kutoka kwa Wazazi wake wawili, kwahiyo Madaktari waliona ni vizuri kutumia mbinu ya matibabu ya mitochondrial donation (MDT), yanayosaidia kumzuia Mama kumrithisha Mtoto magonjwa sugu.


DNA ya Mtoto huundwa kwa kutumia DNA ya Mama na Baba ambayo hutengeneza sifa kuu kama vile tabia zake “personality” pamoja na rangi ya macho lakini kwa upande wa Mtoto huyo alipewa kiasi kidogo cha DNA ya mitochondrial iliyotolewa na Mfadhili wa nje, kisha utaratibu ukafanyika kwa njia ya IVF ambapo yai la Mwanamke likarutubishwa na mbegu ya kiume kwenye maabara na kurudishwa kwenye tumbo la uzazi la Mwanamke ili kukua na kupata Mtoto.

Ikiwa DNA ya mitochondrial itakuwa na tatizo, changamoto mbalimbali zinaweza kusababisha kifo sambamba na matatizo ya moyo, ini kushindwa kufanya kazi, matatizo ya ubongo, upofu na pia matatizo ya misuli yanaweza kumkumba Mtoto huyo.

Mara nyingi magonjwa yanayotokana na hitilafu kwenye mfumo wa DNA hayatibiki na huathiri takribani Mtoto mmoja kati ya watoto 6,500 duniani kote na hivyo njia hiyo imeundwa ili kuzuia Mtoto kuwa na kasoro ambazo wataweza kusambaza kwa vizazi vijavyo na uwezekano wa kuondoa magonjwa hayo mabaya milele.

Ingawa kwa Uingereza hii ni mara ya kwanza lakini sio mara ya kwanza kwa Dunia kushuhudia kisa hiki cha kipekee kwani mwaka 2016 nchini Mexico alizaliwa Mtoto wa kwanza aliyeundwa kwa DNA kutoka kwa Watu watatu kwa usaidizi wa Timu iliyotokea Jijini Newyork nchini Marekani.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 
#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top